KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 30, 2013

Henrique Hilario ajipelekea ziarani Marekani licha ya kuachwa na Chlesea apanda ndege moja na wachezaji wengine

Henrique Hilario huenda akakabidhiwa mkataba mwingine wa mwaka mmoja na klabu ya Chelsea baada ya mlinda mlango huyo aliye nje ya mkataba kusafiri na kufanya mazoezi na watoto wa darajani katika ziara ya maandalizi ya msimu barani Amerika.

Kikosi hicho kutoka London ya kaskazini kimeelekea Marekani hii leo kikiwa na wakali wake kadhaa walioshiriki michuano ya Confederations Cup kama Juan Mata, Fernando Torres, David Luiz, Oscar, Cesar Azpilicueta na John Obi Mikel ambao walikuwa wameongezewa muda wa kupumzika baada ya kurejea kutoka katika michuano hiyo.

 Katika safari hiyo kulikuwepo na sura ya mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 37 ambaye ameungana na walinda mlango wengine Petr Cech, na mlinda mlango kinda Jamal Blackman pamoja na mlinda mlango mpya Mark Schwarzer licha ya kuachwa na timu hiyo baada ya kumalizika msimu uliopita.

Hilario na mlinzi Ross Turnbull kwa pamoja waliondoka katika klabu hiyo yenye maskani yake Stamford Bridge baada ya mchezo wa mwisho wa msimu dhidi ya Everton ambapo mikataba yao ilikuwa imemalizika rasmi. 

Hata hivyo inaonekana kama mlinda mlango huyo mkongwe wa Ureno ambaye alisajiliwa ndani ya klabu hiyo na Jose Mourinho mwaka 2006 wakati huo Mourinho akiwa meneja kwa awamu ya kwanza, huenda akapewa mkataba mwingine wa mwaka mmoja wa kuongeza.

Kikosi cha Mourinho kinajipanga na mchezo wa Ijumaa dhidi ya Inter Milan mchezo wa kirafiki kabla ya kuendelea na ratiba ya michezo mingine iliyo katika ratiba yaoa ya ziara yao ya wiki mbili.

No comments:

Post a Comment