KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 30, 2013

FABIO CAPELLO AELEZEA SABABU YA KWANINI ENGLAND INASHINDWA KUCHUKUA MATAJI.

Bosi wa zamani wa timu ya taifa ya England Fabio Capello ameelezea kushindwa kuchukua mataji makubwa kwa England kuwa kunatokana na ukweli kwamba wachezaji wanakuwa wamechoka sana wanapofikia mwishoni mwa msimu.

Kocha huyo Mtaliano ambaye kwasasa ni kocha wa timu ya taifa ya Urusi, anaamini kuwa kukosokena kwa muda wa kupumzika katikati ya msimu wa ligi kuu ya England  maarufu kama Premier League kunapelekea wachezaji wa England wanaochezea ligi hiyo kujikuta wako tena mashindano katika kipindi cha mashindano makubwa ya kipindi cha Kiangazi.

Alipoulizwa juu ya England kushindwa Capello aliuambia mtandao wa FIFA.COM kuwa ni kwasababu wanakuwa wamechoka kuelekea katika mashindano makubwa

‘Ni kama unapoendesha gari , unaposimama katikati ya safari kuweka mafuta ni dhahiri utafika uendako lakini kama usimami ni wazi kuwa utakuwa unasafiri ukiwa huna mafuta kabla ya kufikia malengo.

‘Maoni yangu ni kwamba michezo inayochezwa katika nusu ya kwanza ya msimu inakuwa ni bora kuliko ya nusu ya pili. Na kwasababu hiyo kama kweli unataka kuwa katika hali ya ushindani katika ligi unahitaji kuwa na kikosi ambacho sehemu kubwa hakitakuwa na wachezaji wa timu ya taifa.’

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 67 amesisitiza kuwa wakati wa uongozi wake England mambo yalikwenda vizuri na kuongeza kuwa 
‘Kilikuwa ni kipindi kilichokwenda vizuri na kwamba inamuuma akikumbuka kichapo cha nchini Afrika Kusini mwaka 2010 dhidi ya Ujerumani katika akisema kikosi kile kilimridhisha sana.

‘Niliwasili wakati timu ikiwa imekosa kufuzu michuano ya Ulaya Euro 2008, lakini chini yangu tulifanikiwa kufuzu kampeni mbili.

‘Rekodi yangu ya kushinda michezo ilikuwa nzuri na pia nilijaza wachezaji vijana kama Danny Welbeck, Jack Wilshere, Phil Jones, Ashley Young, James Milner na Joe Hart.

No comments:

Post a Comment