Meneja wa Manchester United David Moyes anasema mazungumzo ya kumnasa Cesc Fabregas bado yanaendelea.
David Moyes alipokuwa akiongea na wnahabari mjini Osaka, Japan.
Moyes amethibtisha kuwa klabu yake itafanikiwa kumnasa Fabregas na kumpeleka Old Trafford na kwamba klabu yake iko katika mpango wa majaribio wa tatu kwa ajili ya Maestro huyo wa Hispania.
David Moyes ametanabaisha kuwa kuwa Manchester
United's inamtamani Cesc Fabregas kutua Old Trafford na kwamba mipango bado iko hai na mizuri.
Bosi huyo mpya wa United amethibitisha hilo katika mkutano wake na wana habari mjini Osaka, nchini Japan, lakini hakutana kuzungumza mengi juu ya hilo.
Klabu hiyo ilikwisha kuweka mezani kiasi cha pauni milioni 30 kwa ajili ya Fabregas, ambayo ilikataliwa na Barcelona wiki iliyopita.
Kwasasa kiungo huyo bado yuko katika mapunziko baada ya kumalizika kwa michuano ya Confederations nchini Brazil na hakuwepo katika mchezo wa jana ambao Barcelona ilichapwa 2-0 na kikosi meneja Pep Guardiola Bayern Munich.
Wakati huohuo Barcelona imethibitisha kumlipa mafao yake ya sehemu ya mkataba yaliyosalia meneja wao aliyeachia kibarua Tito Vilanova ambaye anasumbuliwa na maradhi ya kansa.
Pep Guardiola aliye iongoza Bayern kushinda mabao 2-0 dhidi ya klabu yake ya zamani Barcelona.
Barcelona imethibitisha kumlipa mafao ya sehemu ya mkataba wake meneja wao wa zamani Tito Vilanova.
No comments:
Post a Comment