Taifa
 Stars imewasili salama hapa Kampala tayari kwa mechi ya marudiano ya 
mchujo dhidi ya Uganda (The Cranes) kuwania tiketi ya kucheza Fainali za
 Tatu za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani 
nchini Afrika Kusini.
Stars
 ambayo iliwasili ikitokea jijini Mwanza ilipokuwa imepiga kambi ya siku
 kumi kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo 
mbili itakwenda Afrika Kusini mwakani imefikia hoteli ya Mt. Zion 
iliyoko eneo la Kisseka katikati ya Jiji la Kampala.
Kocha
 Mkuu wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Kim 
Poulsen ameridhishwa na kiwango cha hoteli hiyo, kwani ndiyo ambayo timu
 ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) ilifikia Novemba mwaka jana 
ilipokuja Kampala kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayoandaliwa 
na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Stars
 ambayo ilitiwa chachu na Rais Jakaya Kikwete alipokutana nayo Uwanja wa
 Ndege wa Mwanza wakati ikiondoka kuja Kampala, na kuitakia kila la 
kheri itafanya mazoezi yake ya mwisho kesho (Julai 26 mwaka huu) Uwanja 
wa Mandela kujiandaa kwa mechi ya Jumamosi.
Kocha
 Kim amesema ingawa mechi hiyo ni ngumu, lakini kikosi chake kimejiandaa
 kuikabili Uganda kwani wachezaji wako wako vizuri na ari kwa ajili ya 
mechi iko juu.
Wachezaji
 wote wako katika hali nzuri, isipokuwa Khamis Mcha aliyekuwa na maumivu
 ya goti, lakini kwa mujibu wa madaktari wa timu anaendelea vizuri kwani
 tayari wanampa mazoezi mepesi.
Kikosi
 cha kamili cha Stars ilichoko hapa kinaundwa na makipa Juma Kaseja, 
Mwadini Ali na Ali Mustafa. Mabeki ni Aggrey Morris, David Luhende, 
Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Nadir Haroub na Vincent Barnabas.
Viungo
 ni Amri Kiemba, Athuman Idd, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Khamis 
Mcha, Mudhathir Yahya, Salum Abubakar na Simon Msuva. Washambuliaji ni 
John Boko, Juma Luizio na Mrisho Ngasa. 
Wakati huo huo, Kocha
 Kim Poulsen atakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari siku ya Jumatatu 
(Julai 29 mwaka huu). Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili asubuhi katika
 ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). 
 


No comments:
Post a Comment