Misri imetanabaisha kuwa itautumia uwanja wa jeshi jijini Cairo watakapo kabiliana na Ghana katika michezo ya mtoano ya hatua ya mwisho kusaka nafasi ya kucheza kombe la dunia.
Itakuwa ni kwa mara ya kwanza Misri ikicheza katika mji mkuu wa nchi hiyo tangu mwezi Oktoba 2011, baada ya vurugu za Port Said ambapo watu kadhaa walitiwa nguvuni baada ya vurugu hizo.
Mfarao hao hivi karibuni michezo yao ililazimika kufanyika huko Red Sea katika uwanja wa El Gouna.
Lakini sasa watakuwa wakihamia katika uwanja ambao una uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000 kuwakabili Ghana.
mchezo huo utapigwa Novemba 19
No comments:
Post a Comment