KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, September 25, 2013

kocha wa Mazembe Patrice Carteron atabiri wachezaji wa kikosi chake kutimkia Ulaya baada ya michuano ya shirikisho Afrika.

Patrice Carteron anatazamia kuwa baadhi ya wachezaji wa kiwango cha juu wa TP Mazembe huenda wakaihama klabu hiyo baada ya michuano ya kombe la shirikisho na kuelekea barani Ulaya.
Mfaransa huyo alichukua kazi ya kuifundisha klabu hiyo ya Jamhuri ya Congo baada ya kuachia ngazi kuifundisha timu ya taifa ya Mali mwezi wa Julai.
Ameichukua klabu hiyo ikiwa na wakali kadhaa wakiwemo Wazambia wawili nyota Rainford Kalaba na Sunzu Stopilla.

Ingawaje hakutaja majina ya wacheza watakao ondoka Carteron amenukuliwa na BBC Sport akisema ana uhakika majina makubwa ndani ya klabu hiyo yataondoka Mazembe baada ya kampeni ya michuano ya kombe la shirikisho.
Mazembe inakabiliwa na michezo miwili ya hatua ya nusu fainali dhidi ya Stade Malien ya Mali, michezo ya nyumbani na ugenini ambayo yote itachezwa mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment