Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Nigeria
Stephen Keshi amesema kukosekana kwa umakini mbele ya goli la wapinzani wao Hispania lilikuwa tatizo kwao
kiasi kupelekea kuondolewa kwao katika michuano ya kombe la shirikisho nchini Brazil.
Mabingwa hao
wa African wamemaliza wakiwa katika nafati ya tatu katika kundi lao baada ya
kukubali kibano cha mabao 3-0 kutoka kwa Hispania mchezo uliopigwa usiku mwingi
kwa saa za Afrika mashariki hiyo jana.
Katika michezo
ya awali ya kundi hiyo Nigeria iliichapa Tahiti kwa mabao 6-1 kabla ya kupoteza
kwa Uruguay kwa kufunga mabao 2-1.
Amenukuliwa keshi
akisema tatizo tumeshindwa kutulia katika eneo la wapinzani, kitu kizuri ni
kwamba tulikuwa tunatengeneza nafasi lakini hatukuwa tukimaliza vema.
"Hicho
ni kitu ambacho tunapaswa kukifanyia kazi. Na ninaimani kukifanyia kazi haraka."
Nigeria ilitakiwa
kushinda katika mchezo huo kusaka nafasi ya kutinga nusu fainali lakini sasa
Hispania wamesonga mbele baada ya ushindi huo wa mabao yaliyofunga mwa Jordi
Alba na Fernando Torres.
Matokeo hayo
yanaifanya Hispania sasa kukutana na Italia Alhamisi katika mchezo wa nusu
fainali ya pili huko Forteleza , ilhali Brazil ikijipanga kukutana na Uruguay
huko Belo Horizonte siku ya Jumatano.
No comments:
Post a Comment