KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, June 24, 2013

Pep Guardiola akubali kuwa yuko katika shinikizo la mataji na kiwango ndani ya Bayern Munich.

 Kocha huyo mwenye umri wa miaka 42 raia wa Hispania alikuwa akiongea katika mkiutano wake wa kwanza kama kocha wa kikosi hicho ambacho mbali ya kuwa bingwa Ulaya lakini pia bingwa wa ligi ya Ujerumani.
Pep Guardiola anaamini na amekubali kuwa yuko katika hanikizo kubwa ndani ya klabu yake mpya ya Bayern Munich kufiakia mafanikio yaliyofikiwa nammtangulizi wake Jupp Heynckes.
Amenukuliwa akisema
"Nina matumaini ya kulinda kiwango cha timu kilichoonyeshwa msimu uliopita" 

Guardiola aliiacha Barcelona na kujipa mapumziko ya mwaka mzima baada ya msimu wa mwaka 2011-lakini pia akawashangaza wengi baada ya mwezi January kuibuka na kukubali mkataba wa miaka mitatu na Bavarian akianazia na kiangazi hii.

Chini ya meneja mwenye umri wa miaka 68, Heynckes klabu hiyo ya Bayern imekuwa ni klabu ya kwanza kunyakua mataji matatu kwa mpigo ikiwa ni pamoja na taji la ligin kuu ya Ujerumani Bundesliga, European Cup na kombe la Ujerumani ndani ya msimu mmoja

No comments:

Post a Comment