Ghana na Nigeria zimetakiwa kujitahidi na kujirekebisha endapo zitahitaji kufanya
vema katika michuano ya kombe la dunia kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka
20 fainali zake zikifanyika nchini Uturuki baada ya zote kuanza kwa vichapo.
Bingwa wa
zamani Ghana alianza kwa kutereza mbele ya Ufaransa baada ya kukubali chapo
cha mabao 3-1 kutoka kwa Ufaransa ilhali Nigeria wakikubali mbele ya Ureno kwa
kichapo cha mabao 3-2.
Kocha wa Ghana
Sellas Tetteh, ambaye aliipa Ghana ubingwa mwaka 2009 amelalamikia sehemu yake ya
ulinzi ya timu yake kuwa ilikuwa na tatizo.
Ufaransa
waliapata bao la utangulizi kupitia kwa Geoffrey Kondogbia, kabla ya Yaya
Sanogo kuongeza la pili muda mfupi baadaye.
Christophe
Bahebeck aliandika bao la tatu kabla ya Yiadom Boakye kufunga bao la kufuatia
majonzi kwa upande wa Black Satellites.
Kocha wa Nigeria
Obuh, anasema anautaza mchezo ujao dhidi ya Cuba, baada ya kupokea kichapo cha
kwanza kutoka kwa Ureno.
No comments:
Post a Comment