Andrey Arshavin |
Andrey Arshavin: Zenit St Petersburg
yamsajili mshambuliaji wa zamani wa Arsenal.
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Andrey Arshavin amerejea katika klabu yake ya zamani ya Zenit St Petersburg kwa mkataba wa miaka miwili.
Arshavin mwenye umri wa miaka 32 alielekea katika viunga vya Emirates kwa mkataba ulioripotiwa wa pauni milioni £15 mwezi January mwaka 2009, lakini amejumuioshwa katika orodha ya wachezaji 14 ambao wametangazwa kutokupewa mikataba mipya msimu ujao wa ligi kwa washika mitutu hao.
Rai huyo wa Urusi ameitumika Arsenal ya England katika kipindi cha miaka mitano.
Taarifa ya Zenit inasema
"Miongoni mwa wachezaji bora nchini Urusi katika kipindi cha muongo uliopita anarejea nyumbani"
Arshavin
aliaanza kuitumikia Zenit mwezi August 2000 katika mchezo ambao timu hiyo ilishinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Bradford City katika michuano ya Intertoto Cup.
Arshavin
alikuwa katika kipindi cha mafanikio ndani ya klabu hiyo aliyoitumikia kwa miaka tisa ambapo alikuwemo katika timu ya ushindi wa taji la Uefa Cup mwaka 2008 baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Rangers.
Isco: Real Madrid yaizidi kete City kwa kumnasa Isco
Real Madrid
imefikia makubaliano na Malaga kwa ajili ya kumasajili Isco kwa mkataba wa miaka mitano kwa ada iliyoripotiwa ya pauni milioni £23m.
Manchester
City pia ilikuwa katika mbio za kumfukuzia kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 huku meneja mpya wa klabu hiyo Manuel Pellegrini
akiwa na matumaini ya kumnasa na kumpeleka England .
Isco, ambaye hivi karibuni alishinda taji la Ulaya akiwa katika kikosi cha Hispania cha Under-21 katika michuano ya European Championship anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya July 3 kabla ya kutambulishwa Bernabeu.
Anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na meneja mpya wa Real Madrid Carlo Ancelotti.
Isco alisajiliwa na Pellegrini akitokea Valencia mwaka 2011 pia anadhani angependa kumtumia tena msimu ujao ambapo yeye Isco amemtaja meneja huyo kama baba yake wa soka "footballing
father".
Danny Simpson: QPR yajipanga kusajili mlinzi wa Newcastle Danny Simpson
QPR imekubali kusajili mlinzi Danny Simpson kwa mkataba wa miaka mitatu kufuatia mlinzi huyo kuachiwa huru na klabu yake ya Newcastle.
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 26 atakuwa akijiunga QPR Julai mosi baada ya maafikiano kufikiwa juu ya mkataba wake wa sasa na Newcastel .
Simpsonamezungumza kupitia mtadao wa klabu yake mpya akisema
"Harry
Redknapp ni meneja wa kiwango cha juu na nimeongea naye na huu ni uhamisho sahihi kwangu.
"Siku zote nimekuwa nikimpenda. Ni mtu mkubwa katika soka na ninamuheshimu sana"
Simpson aliyejifunza soka katika klabu ya Manchester United huko nyuma ameitumikia Newcastle kwa michezo 137 baada ya kujiunga katika viunga vya Tynesiders, hapo kabla kwa mkopo August 2010.
No comments:
Post a Comment