Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Robert Lewandowski amethibitisha kuwa atajiunga na Bayern Munich mwakani.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anaweza kusaini mkataba wa awali (pre-contract) mwezi wa January kuelekea kukamilisha uhamisha huru wakati wa majira ya kiangazi lakini akiwa na matumaini ya kuhamia katika klabu hiyo wakati wa uhamisho wa majira ya baridi.
Amenukuliwa mshambuliaji huyo na kituo cha televisheni cha Sport 1 akisema
Lewandowski alifunga jumla ya mabao 36 akiwa na Dortmund msimu uliopita.
Ilikuwa ikidhaniwa kuwa angehama kuelekea kwa mabingwa hao wa Ujerumani na Ulaya na alipoulizwa kama angeweza kuthibitisha kuwa mwakani anaondoka alijibu
"Yes, because then I can officially sign a contract."
Majira ya kiangazi yakiyopita kiungo wa Kijerumani Mario Gotze aliihama Dotmund na kujiunga na Munich kwa uhamisho wa pauni milioni 31.5.
No comments:
Post a Comment