Mashindano ya magongo kwa mataifa ya Afrika
yaliyopangiwa kuanza Alhamisi wiki hii mjini Nairobi huenda
yakaahirishwa kutokana na mkasa wa jumba la Westgate lililovamiwa na
magaida wa Al Shabaab, na zaidi ya watu sitini kuuawa
Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa magongo cha
Kenya Nashon Randiak anasema shirikisho la kimataifa,FIH, lina wasiwasi
kuhusu usalama wa wachezaji mjini Nairobi baada ya magaidi wa Al Shabaab
kulivamia jengo la kibiashara la Westgate jijini Nairobi.
Licha ya Randiak kuwaeleza kwamba
hali sasa ni shwari baada ya magaidi wote kuuwa na wanajeshi wa Kenya
shirikisho la kimataifa limesema linataka mkuu wa polisi nchini Kenya
kuwahakikisha usalama wa wachezaji.
Randiak ameshangazwa na msimamo huo akisema
mashambulizi ya magaidi hutokea kote duniani hivyo anashangaa ni kwanini
hili la Kenya linachukuliwa ni kama la kipekee.
Mataifa yanayotarajiwa kushiriki kwa wanaume ni
Kenya, Ghana na Afrika Kusini na kwa wanawake ni Kenya, Tanzania,Ghana
na Afrika Kusini. Timu ya Tanzania ikiongozwa na katibu wa chama cha
magongo mkoa wa Dar es salaam Mnonda Magani tayari imeshawasili mjini
Nairobi.
Timu ambazo zimejiondoa kwa sababu mbali mbali na sio hiyo ya Westgate ni pamoja na Nigeria, Namibia, Misri na Ushelisheli.
No comments:
Post a Comment