Dereva wa magari ya Timu ya Mecedes Lewis Hamilton ameweza kuishindia timu yake ushindi wake binafsi wa kwanza kwa Mercedes kwa kuongoza tangu mwanzo na kuwazidia madereva wenzake kwenye mashindano ya Hungary ya mbio za magari ya Langalanga au Formula 1.
Hamilton alijituliza na kutumia kasi akiwashinda
dereva Kimi Raikkonen wa Timu ya magari ya Lotus aliyemaliza wa pili na
Sebastien Vettel wa Red Bull aliyemaliza wa tatu.
Mark Webber wa Red Bull alionyesha
umahiri wake kwa kujikwamua kutoka nafasi ya kumi alikoanzia mashindano
hadi kumpiku dereva moto moto wa Timu ya magari ya Ferrari, Fernando
Alonso.
Kutokana na hali hio Raikkonen sasa anapanda kwa
pointi moja mbele ya Alonso akishika nafasi ya pili kwa jumla ya pointi
alizokusanya tangu kuanza kwa mashindano ya msimu huu wa 2013/2014
ingawa bado yuko nyuma ya kiongozi wa mashindano na mtetezi wa taji
Sebastien Vettel kwa pointi 38.
Kwa kipindi kirefu cha mashindano haya Fernando
Alonso alikua katika jitihada za kuzuia asipitwe na Romain Grosjean wa
timu ya Mercedes, na katika pilikapilika Romain Grosjean, alijitia
matatani na kuadhibiwa kwa kupita gari akizunguka nje ya uwanja.
Wakati huo alimpita Felipe Massa wa Ferrari
kwenye mzunguko wa 29 kituo cha nne, ambapo tairi zote nne zilivuka
msitari mweupe unaobainisha uwanja na papo hapo kupewa adhabu ya
kuuzunguka uwanja.
Hapo jana baada ya Hamilton kushinda nafasi ya
mbele ya kuongoza mbio za leo alisema kua utakua muujiza endapo
atashinda ikizingatiwa hali ya joto kali nchini Hungary bila kusahau
matatizo yaloikumba timu ya magari ya Mercedes kwa matairi kupasuka kila
mara.
Lakini alidhibiti mashindano kwa mda wote
akipoteza uongozi kwa Grosjean na baadaye Mark Webber aliposimama
kubadili tairi na mafuta lakini aliweza kurudi kileleni pale Webber
aliposimama kubadili tairi na mafuta.
No comments:
Post a Comment