Wayne Rooney atarejea Manchester United mwezi August anasema David Moyes.
David Moyes wa United akishuhudia vijana wake wakitoteshwa na Yokohama F-Marinos hii leo na kufungwa jumla ya mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki huko Tokyo.
Meneja wa Manchester United David
Moyes ameendelea kuelezea kuwa mshambuliaji wake Wayne Rooney hayuko sokoni na kwamba mshambuliaji wake huyo atarejea katika kikosi chake katika mchezo wa kirafiki huko Stockholm Agosti 6.
Akizungumza hii leo baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Yokohama huko Tokyo, Moyes ameweka wazi kuwa Rooney anaendelea kupata nafuu ya jeraha lake la msuli ambalo lilimrejesha nyumbani katika ziara yao inayoendelea na kwa mara nyingine amesisitiza kuwa mshambuliaji huyo hataruhusiwa kuondoka katika klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford.
Moyes amenukuliwa akisema kuwa
'Ndio anaendelea vizuri na anafanya mazoezi mepesi ya kukimbia na hiyo ndio habari nianyo ipata kutoka nyumbani kuwa anaendelea vizuri. Tulishasema hauzwi na hilo halitabadilika.'
Rooney aliripotiwa kuwa ni mwenye hasira na hafurahii maisha yake Old Trafford, baada ya Sir Alex Ferguson kudai mwishini mwa msimu uliopita kwamba mshambuliaji huyo ameonyesha nia ya kuondoka Manchester United.
No comments:
Post a Comment