Kikosi cha Young Africans kilichoanza katika mchezo wa leo dhidi ya timu ya Rhino Rangers. |
Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara timu ya Young Africans imetoka
suluhu ya bila kufungana na timu ya Rhino Rangers katika mchezo
uliofanyika jioni hii katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora
na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa washabiki.
Young Africans ambayo ilikua ikicheza mchezo wake wa mwisho baada ya
kucheza michezo miwili ya awali dhidi ya timu ya Express ya kutoka
nchini Uganda ambapo ilitoka sare mchezo mmoja na kufungwa mmoja.
Jerson
Tegeta aliipatia Young Africans bao dakika ya kwanza ya mchezo lakini
katika hali ya kutatanisha mwamuzi wa mchezo huo alikataa bao hilo hali
iliyowafanya washabiki waliofurika katika uwanja huo kumzomea mwamuzi.
Rhino
Rangers iliyopanda ligi kuu msimu huu ilifanya mabadiliko haraka haraka
katika dakika 30 za mwanzo ambapo ilikua imezidiwa sehemu ya kiungo
pamoja na mabadiliko hayo bado vijana wa jangwani waliendelea kuutawala
mchezo huo.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 0 - 0 Rhino Rangers.
Kpindi
cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ambapo Young
Africans ilimtoa kiungo Hamis Thabit na nafasi yake ikichukuliwa na
Abdallah Mnguli ambaye alisaidia kuongeza kasi ya mashambulizi.
Mipira
miwili iliyorushwa na mlinzi Mbuyu nusura iipatie Young Africans bao
lakini kutokua makini kwa washambuliaji wake kuliwafanya kupoteza nasi
hizo za wazi.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 0 - 0 Rhino Rangers.
Young Africans: 1.Deogratius
Munishi 'Dida', 2.Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4.Mbuyu Twite, 5.Rajab
Zahir/Ibrahim Job, 6.Salum Telela, 7.Nizar Khalfani, 8.Hamis
Thabit/Abdallah Mnguli, 9.Didier Kavumbagu, 10.Jerson Tegete/Shaban
Kondo, 11.Said Bahanuzi
No comments:
Post a Comment