Suarez (kushoto) akishangilia na mshambuliaji mwenzake Diego Forlan baada ya kufunga goli safi la tatu.
Sakata la Luis Suarez limeingia katika sura mpya kufuatia kulishwa maneno na mwandishi wa habari wa gazeti la nchini Uruguay la El Observador ambaye alimnukuu mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay akisema anataka kusalia katika klabu yake ya Liverpool.
Inavyoonekana ni kwamba mshambuliaji huyo amekanusha kauli iliyonukuliwa kwa kichwa cha habari ‘For now, owing to all the affection of the people, I would be staying.’Lakini baada ya mchezo ambao Uruguay ilishinda kwa mabao 4-2 dhidi ya Japan jana mchezo ambao Suarez alifunga goli mshambuliaji huyo aliripotiwa akisema sikusema hivyo. Pengine kuna mtu mwingine aliyesema hayo na kubwa zaidi ni kwamba niko hapa na timu na timu ya taifa.
No comments:
Post a Comment