KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 15, 2013

PATA PICHA YA LIGI YA ENGLAND KABLA YA KUANZA MWISHONI MWA JUMA.


Big shoes: Manchester United's new boss David Moyes has replaced Sir Alex Ferguson after 27 years
David Moyes
The return: Jose Mourinho is back in charge at Chelsea

Baada ya muda mrefu wa kipindi cha kiangazi hatimaye msimu umerejea. Msimu mpya wa ligi kuu ya soka nchini England Barclays Premier League unaanza mwishoni mwa juma hili kwa mtazamo wa kuwa  ni msimu bora kufuatia mabadiliko makubwa katika vilabu mbalimbali.

Manchester United baada ya miaka 27 ya mafanikio ya mataji 38 chini ya aliyekuwa meneja wa klabu hiyo kabla ya kiangazi Sir Alex Ferguson alijuuzulu nafasi yake ya kuiongoza benchi la ufundi la  Old Trafford. David Moyes amekuwa ndiye mbadala wake baada ya bosi wa zamani wa Everton kupewa nafasi hiyo na mzee Fergie.
 
Swali ni je United itaweza kutwaa taji chini ya Mscochi mwingine? Wakati hatima ya mshambuliaji Wayne Rooney ikiwa mashakani unaonekana wazi kuwa hautakuwa mwanzo mzuri wa msimu kwa Moyes.

Katika jiji hilohilo la Manchester klabu nyingine ya Manchester City iliachana na aliyekuwa meneja wake Roberto Mancini baada ya kushindwa kutwaa taji ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Manuel Pellegrini.

Kikosi cha timu hiyo kina sura za wachezaji wapya kadhaa ambapo klabu hiyo imetumia kiasi cha pauni milioni £90 kwa kuwasajili Fernandinho, Alvaro Negredo, Stevan Jovetic na Jesus Navas. Presha kubwa itakuwa ikielekezwa kwa Pellegrini kulirejesha taji la ligi kuu ya Premier katika viunga vya Etihad.

Klabu tishio ambayo inaonekana ni tatizo kwa vilabu hivyo kutoka katika jiji la Manchester ni Chelsea, ambayo majira ya kiangazi imeshuhudia kurejea kwa 'Special One', Jose Mourinho.

Kurejea kwa mreno huyo ni kama kumeasha upya nafasi yao ya kuwa ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi ya kuweza kutwaa taji kufuatia pia uwekezaji uliofanywa kwa Andre Schurrle na Marco van Ginkel. Klabu hiyo bado inamfukuzia Rooney na huenda saini yake ikawa ni nguvu ya kutosha kuondoa uwezekano kwa vilabu vya jiji la Manchester kutwaa taji London.
Luis Suarez
Luis Suarez
Wayne Rooney
Wayne Rooney
Gareth Bale
Gareth Bale

Vita ya nafasi ya nnne za juu inaonekana kuwa ni kubwa zaidi huku Tottenham ikiwa imejipanga kuweza kuondoa tofauti iliyojitokeza ya alama moja na Arsenal.

Lakini inavyoonekana ni kwamba kazi kubwa ya kuwachukua Paulinho, Nacir Chadli na Roberto Soldado inaweza ikawa ni bure kama Gareth Bale ataamua hatama yake ya baadaye sehemu nyingine.

Mashabiki wa Arsenal kwa mara nyingine wameonekana kuchanganyikiwa na kutokuwepo na shughuli za uhamisho katika majira ya kiangazi . Uhamisho huru wa Yaya Sanogo kutoka katika klabu ya Auxerre ndio uhamisho pekee uliokamilishwa licha ya kwamba jaribio la kunasa saini ya Luis Suarez kutoka Liverpool likiendelea.
 Big spenders: Manchester City have spent £90m, and installed Manuel Pellegrini at the helm, to try and recapture their Premier League title

Big spenders: Manchester City have spent £90m, and installed Manuel Pellegrini at the helm, to try and recapture their Premier League title.

Gary Medel
Ricky Van Wolfswinkel

Investment: Norwich have spent well, bringing in Ricky van Wolfswinkel (left), while Cardiff City have broke their transfer record three times as they try to stay in the Premier League - Gary Medel (left) cost £11m

Uwekezaji mkubwa wa wachezaji pia umefanywa na klabu ya Norwich City ikisaka kumaliza katika nafasi za juu msimu huu, huku Aston Villa na Sunderland zikifanya mabadiliko kadhaa katika kujaribu kuimarisha kinafasi katika msimamo wa ligi tofauti na msimu uliopita.

Klabu mpya iliyopanda ya Cardiff City imefanya mabadiliko makubwa ya uhamisho wa rekodi ya klabu mara tatu huku Palace ikivunja benki yao fedha kwa kumchukua Dwight Gayle kutoka Peterborough. Steve Bruce amefanya usajili wa makini ambao bila shaka utaisaidia kikosi chake cha Hull City kufanya vema.

Kwingineko, meneja wa siku nyingi wa Stoke City Tony Pulis aliondoka katika klabu yake hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na Mark Hughes naye Roberto Martinez akienda kuziba pengo la David Moyes katika klabu ya Everton. Newcastle United hatimaye ikamsajili Loic Remy.


No comments:

Post a Comment