KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, September 19, 2013

Andy Murray hoi sasa kusubiri mwakani kifundo cha nyuma cha mguu chamaliza ndoto zake.

Andy Murray hategemewi kucheza tena msimu huu baada ya kuamua kufanyiwa upasuaji katika kifundo cha mguu tatizo lililokuwa likimsumbua kwa muda mrefu.
Marry mwenye umri wa miaka 26 alipatwa na matatizo hayo ambayo sasa yatamuweka nje ya mashindano kwa sehemu yote iliyosalia ya mwaka ikiwa ni pamoja na michezo ya fainali ya mwezi Novemba ya Tour mjini London.
Majeraha hayo aliyapata mapema mwezi wa Mei ambayo yalimnyima nafasi ya kucheza michuano ya French Open.

Alirejea mwezi Julai na kuibuka kuwa Mwingereza wa kwanza kushinda taji la Wimbledon tabngu mwaka 1936 lakini alishindwa kufanya vema katika robo fainali ya michuano ya US Open.

Murray alikuwa ana ratiba ya kushiriki michezo zaidi ya Asia msimu huu ikiwa ni pamoja na kule China katika michuano ua Shanghai Masters na baadaye kueleka katika michuano mingine ya Paris Masters kabla ya kuelekea katika fainali ya World Tour ambayo inatarajiwa kufanyika mwezi Novemba katika ukumbi unatambulika kama O2 Arena.

No comments:

Post a Comment