Tiger Woods anasema kuwa anatarajia kushinda taji lake la sita
mwishoni mwa mwaka na kujishindia dola milioni sita nukta tatu katika
mashindano ya Tour yanayoanza Alhamisi.
Bingwa huyo wa dunia ni mmoja wa wachezaji
watano wanaojua kuwa ushindi katika mashindano hayo mjini Atlanta
yatawapa nafasi ya kujishindia kombe la FedEx Cup kwa msimu wote, wakati
wachezaji watakaosali wanaweza pia kujipatia kitita cha ziada.
''Ushindi wangu mara tano mwaka huu, umekuwa jambo nzuri kwangu,'' alisema Woods.
"kama wachezaji wenzangu wanne walio katika nafasi za kwanza tano, tunajitahidi kujitengezea mustakabali wetu.''
Aliongeza kusema kuwa: '' nadhani nimecheza
vyema sana. Nimeshinda mara mbili na nimemaliza wa pili mara nne. Hiyo
sio vibaya katika maisaha yangu kama mchezaji wa Golf.''
Henrik Stenson, Adam Scott, Zach Johnson na Matt
Kucharni wachezaji wengine wanaojua kuwa ushindi utawaweka katika
nafasi nzuri kuwawezesha kupata kitita hicho wakati Woods anaweza
kumaliza katika nafasi ya 29 na bado aweze kuwa katika nafasi ya
kushinda.
Kwa bingwa wa mashindano ya Open Phil Mickelson
kuweza kushinda , anahitaji kushinda mashindano haya ambayo yenyewe yana
zawadi ya dola milioni 1.4.
Bingwa wa Uingereza Justin Rose anahitaji kuwa katika hali sawa na hiyo.
No comments:
Post a Comment