Jose Mourinho |
Meneja wa klabu ya Chelsea Jose
Mourinho anasema yeye ndiye anayepaswa kuwajibika kufuatia kipigo cha
timu yake ilipochuana na Basel kutoka Uswizi 2-1 katika mechi ya Ligi ya
mabingwa barani Ulaya.
Alikua mcheza kiungo Oscar aliyeifungulia
Chelsea bahati ya uwezekano wa kushinda mechi hiyo lakini Mohamed Salah
akarudisha kabla ya Marco Streller kufunga kwa kichwa bao la ushindi kwa
Basel.
"tunaposhindwa sizungumzii wachezaji au mtu binafsi, huzungumzia jukumu langu," alisema Mourinho. "anayewajibika ni mimi."
Nyota aliyesajiliwa hivi karibuni Samuel Eto'o
alianza mechi huku mshambuliaji Demba Ba kuletwa baadaye katika kipindi
cha pili, huku mshambuliaji mwingine Fernando Torres hakua hata kwenye
meza ya wachezaji waliorodheshwa.
Hata hivyo meneja huyo kutoka Ureno alisisitiza
kua hana wasiwasi juu ya kikosi chake hususan washambuliaji wake, licha
ya ukosefu wa magoli.
"ninawaamini washambuliaji wangu watatu kwa msimu mzima," Aliongezea Mourinho.
Mshambuliaji mkongwe kutoka Cameroon Samuel
Eto'o aliyehamia kutoka klabu ya Urussi Anzhi Makhachkala, lakini
hakumsumbua golikipa wa Basel Yann Sommer hadi kipindi cha majeruhi.
No comments:
Post a Comment