Thamani ya haki ya mauzo ya sura na hadhi ya mchezaji imefikia
viwango vikubwa ikilinganishwa na enzi zile kabla ya dereva wa magari
ya mbio za magari ya Langalanga Eddie Irvine kujinyakulia pauni 25,000
kutoka kituo cha Redio moja iliyotumia picha yake kutangazia biashara
bila idhini yake mnamo mwaka 1999.
Enzi hizo picha za wanamichezo maarufu zilionekana kama mali ya umma.
Lakini
michezo ilipozidi kuwa maarufu kote duniani, umuhimu wa hati miliki za
michezo na wachezaji wake kama chombo cha kuuzia bidhaa na wahusika
wenyewe kunufaika na taaluma yao.
Nyota wa michezo kama David Beckham, Cristiano
Ronaldo, na sasa Gareth Bale wote wamefaidi mapato makubwa yanayoweza
kupatikana kupitia masoko ya kuuza bidhaa kama chupi na viatu.
"wanamichezo wamegundua uwezekano walio nao wa
kufaidi kupitia haki zao, anasema Nigel Currie wa kampuni ya mauzo ya
vifaa vya michezo Brand Rapport.
"hati miliki inaweza kutegemea mtu binafsi na juhudi zake Bale.
"lililo bayana ni jina mfano kama Gareth Bale,
na ikiwa jina lako lipo kwenye jezi ya mchezo wa soka, hapa unapatia
hati miliki moja kwa moja."
Kijana kutoka Wales Bale mwenye umri wa miaka
24, aliyehamia klabu ya Real Madrid kwa kitita cha pauni milioni £85m,
anatazamiwa kuunda mamilioni ya fedha kupitia hati miliki ingawa tayari
asili mia 50 itahifadhiwa na klabu ya Uhispania.
No comments:
Post a Comment