Siku chache tu baada ya kutumia
kitita kikubwa kumsajili Gareth Bale kutoka klabu ya Tottenham hotspurs
ya England Real Madrid imetangaza kupanda kwa faida katika mapato yake
na punguzo la asilimia 27.4 ya deni lake katika kipindi cha msimu wa
mwaka 2012/13.
Magwiji hao wa soka ya Uhispania wameshuhudia mapato yao
yakipanda mpaka kufikia Euro milioni 520.9.
Mapato hayo hayahusishi udhamini mkubwa wa Fly
Emirates wa shati za klabu unaokadiriwa kuwa euro milioni 29 kwa kila
mwaka kuanzia msimu huu.
Pamoja na usajili wa Bale, Real ilitumia euro milioni 70 kwa kuwapata Isco na Asier Illarramendi.
Vilevile klabu hio ilirejesha takriban euro
milioni 100 katika kuwauza wachezaji wake Mesut Ozil aliyejiunga na
Arsenal kunako siku ya mwisho wa usajili na Gonzalo Higuain, Raul Albiol
na Jose Maria Callejon waliojiunga na Napoli mwezi julai.
Uwamuzi wa Kaka kuondoka Real Madrid na kurudi
AC Milan pia kulipunguza kiwango cha mishahara ya klabu hiyo kwa
mshahara wake wa euro milioni 10 kwa mwaka wake wa mwisho lau kama
angehitimisha mkataba wake.
No comments:
Post a Comment