Shirikisho la soka nchini Gabon (Fegafoot) limemfukuza kazi kocha wa kikosi cha timu ya taifa hilo mreno Paulo Duarte kufuatia nchi hiyo kuondolewa katika kinyanganyiro cha kusaka nafasi ya kucheza kombe la dunia 2014.
Fegafoot imemfukuza kazi Duarte hapo jana lakini ataendelea kusalia shirikisho hilo katika kazi ya mkurugenzi wa ufundi mpaka April.
Duarte aliajiriwa kazi kwa mkataba wa miaka miwili mwezi April mwaka uliopita akitokea nchini Ujerumani Gernot Rohr, na akiwa nchini Gabon alikiongoza kikosi wakati wakiwa waandaaji wa michauano ya mataifa ya Afrika 2012 pamoja na Mali.
Gabon ilivutia katika michuano hiyo na kufika hatua ya robo fainali na kucheza soka safi kabla la kushambulia kabla ya kupoteza kwa Mali kwa njia ya mikwaju ya penati.
Duarte alishindwa kuisaidia timu kujenga kiwango kiasi kupelekea kushindwa kuingia katika fainali za mataifa ya Afrika mwaka huu na kumaliza katika nafasi ya tatu katika kundi katika michezo wa kufuzu kombe la dunia.
No comments:
Post a Comment