Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga (katikati) akiongea na waandishi wa habari , kulia ni Mohamed Bhinda (mjumbe wa kamati ya utendaji) , kushoto Baraka Kizuguto Afisa Habari. |
Makamu mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Clement Sanga leo
amefanya mkutano na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi juu ya habari
zilizokuwa zimeenea kuhusiana na taarifa za mabadiliko ya kaimu katibu
mkuu Lawrence Mwalusako kuondolewa kwenye nafasi yake na kuchukukuliwa
na mtu mwingine.
Akiongea na waandishi wa habari Sanga amesema taarifa hizo hazina
ukweli kwamba tayari kuna mtu anachukua nafasi ya Mwalusako, bali
kilichotokea ni kutokuwepo kwa mawasiliano mazuri katika suala hilo kati
ya viongozi na wazee.
Kilichopo ni kwamba uongozi wa klabu ya
Young Africans upo katika mchakato wa kuhakikisha unajaza nafasi
zilizopo wazi za mkurugenzi wa ufundi, mkurugenzi wa masoko, mkurugenzi
wa fedha na zoezi hilo linaendeshwa na kampuni moja ambayo waliipa
nafasi ya kuendesha zoezi hilo.
Zoezi likiwa ndani ya mchakato
mmoja wa waombaji wa nafasi hizo Patrick Naggi aliwasili makao makuu ya
klabu ya Yanga kwa lengo la kutaka kujua mazingira ya ufanyaji kazi
yakoje na kufahamu baadhi ya mambo kuhusiana na klabu ndipo kulipotokea
kutokuelewana na baadi ya wanachama wakiwemo wazee waliokuwepo eneo la
klabu.
Kwa maana hiyo napenda kutoa taarifa kwa umma na wanachama
wa Yanga kuwa uongozi bado haujatoa baraka za ajira kwa mtu yoyote
katika nafasi hizo, isipokuwa ni muombaji aliwahi kufika makao makuu
kabla ya mchakatao wa usahili kukamilika.
Lawrence Mwalusako
anaendelea kuwa kaimu katibu mkuu wa Yanga mpaka hapo kutakapokuwa na
taarifa nyingine zozote za mabadiliko kwa nafasi zote zilizopo wazi
katika idara mbalimbali.
Uongozi unawaaomba wanachama, wapenzi na
washabiki wa soka kuwa kitu kimoja katika kuunga mkono harakati za
kimaendeleo ili kuifanya timu iende katika hatua nyingine ya ushindani
wa kimatifa.
No comments:
Post a Comment