Qatar imesisitiza kuwa inaweza kuandaa dimba la Kombe la Dunia mwaka wa
2022 katika majira ya joto, hata wakati Shirikisho la FIFA likiendelea
kuwekewa mbinyo wa kuhamisha tamasha hilo hadi msimu wa baridi
Taifa hilo lenye utajiri wa nishati, ambako nyuzijoto hufikia sentigredi
45 ilipewa kibali cha kuandaa Kombe la Dunia miaka mitatu iliyopita
katika uamuzi wa kushangaza.
Qatar inasema inaweza kukubali kuhamisha dimba hilo hadi msimu wa baridi
lakini ikasisitiza kuwa licha ya joto kali, inaweza kuandaa Dimba la
Dunia msimu wa joto kwa kujenga viwanja vyenye hewa ya baridi kwa
kutumia teknolojia mpya inayojali mazingira.
Namna ambavyo mashabiki wataweza kukabiliana na joto, nje ya viwanja,
bado ni suala linalotia wasiwasi na Rais wa FIFA Sepp Blatter hivi
karibuni amesema lilikuwa kosa kupanga kinyang'anyiro hicho cha msimu wa
joto, katika taifa la jangwa.
Rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA, Michel Platini pia
amethibitisha kuwa mashirkisho 54 wanachama wa UEFA wamekubaliana kwa
kauli moja kuhusu wazo la kuhamisha dimba hilo la Qatar, hadi msimu
mwingine wa mwaka
Lakini nayo kamati andalizi ya Qatar imejaribu kuondoa wasiwasi hiyo,
kwa kusema teknolojia ya kuleta hewa ya baridi, kwa kutumia solar,
katika maeneo ya umma, nje na ndani ya viwanja, huenda ikatatua shida
hizo. bila shaka tutasubiri kuona jinsi namna suala hilo
litakavyokwenda, nasi tutakufahamisha
No comments:
Post a Comment