KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, October 21, 2013

Bayern yarejea kileleni mwa Bundesliga

Bayern Munich imerejea katika kilele cha ligi kuu ya nchini Ujerumani Bundesliga baada ya Bayer Leverkusen kuchukua usukani kwa muda wakifaidika na goli hewa dhidi ya Hoffenheim siku ya Ijumaa. 
Katika mchezo wa kuvutia hiyo jana Jumapili kati ya Hamburg SV na VFB Suttgart, vigogo hivyo vya soka la Ujerumani vilitoshana sare ya mabao 3-3. 
Na katika mchezo wa mwisho jana jioni uliofikisha mchezo wa roundi ya 9 ya Bundesliga , Wolfsburg ilishinda baada ya kuonesha mchezo dhaifu katika kipindi cha kwanza dhidi ya Augsburg na kujipatia points tatu za kwanza ugenini. VFL Wolfsburg ilipata ushindi wa mabo 2-1.
Mabingwa watetezi wa Bundesliga Bayern Munich walirejea kileleni mwa ligi hiyo wakiipora nafasi hiyo kutoka kwa Leverkusen. Kikosi cha Leverkusen kilifadika na bao hewa la Kießling siku ya Ijumaa dhidi ya Hoffenheim. BVB , Borussia ilipata ushindi wa taabu wa bao 1-0 dhidi ya Hannover kama ilivyokuwa kwa Schalke 04 ambao walikuwa wageni wa wageni katika ligi hiyo Braunschweig ambao Schalke ilipata ushindi wa kubana wa mabao 3-2.
Borussia Dortmund yapata ushindi mwembamba dhidi ya Hanovver
Nürnberg na Freiburg zilitoshana sare ya bao 1-1, lakini bado zimeshindwa kupata ushindi. Siku ya Jumamosi Hertha BSC Berlin iliishinda Gladbach kwa bao 1-0 na kuchupa hadi nafasi ya nne.

Kwingineko katika bara la Ulaya ,
Mabingwa wa La Liga ligi ya Uhispania Barcelona walishindwa kuuona wavu siku ya Jumamosi kwa mara ya kwanza katika michezo 65 iliyocheza baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Osasuna.
Atletico Madrid ikakubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Espanyol wakati Real Madrid iliibuka kidedea kwa kupata ushindi wa tisa mfululizo.
Fans von Real Madrid singen am 24.04.2013 in der Innenstadt von Dortmund (Nordrhein-Westfalen). Am Abend findet im Signal-Iduna-Park das UEFA Champions League Halbfinalspiel von Borussia Dortmund gegen Real Madrid statt. Foto: Kevin Kurek/dpa Mashabiki wa Real Madrid

Fiorentina iliirarua Juventus Turin kwa mabao 4-2 baada ya kuwa nyuma kwa mabao 2-0, na kuipa Juventus kipigo chake cha kwanza msimu huu katika Serie A nchini Italia.
AS Roma nayo ikainyoa bila maji SSC Napoli kwa mabao 2-0.
Nchini Uingereza Arsenal London imeongeza uzito katika kampeni yake ya kuwania ubingwa msimu huu baada ya kuweka wavuni mabao 4 dhidi ya Norwich City wakati mchezaji wa kati Mesut Ozil akionesha uwezo mkubwa wa kuiunganisha timu hiyo. Arsenal iko points mbili juu ya msimamo wa ligi ikifuatiwa na Chelsea.
GettyImages 143320446
HAMBURG, GERMANY - NOVEMBER 14: Mesut Oezil of Germany poses during a national team photocall on November 14, 2011 in Hamburg, Germany. (Photo by Oliver Hurst - Pool/Bongarts/Getty Images) Mesut Özil

Manchester City na Tottenham Hotspurs zilipata ushindi mwishoni mwa juma, lakini hali ya wasi wasi inawakumba mabingwa watetezi Manchester United baada ya kushindwa kupata kama kawaida yao ushindi wa kufuatana na kuiacha timu hiyo ikiwa katika nafasi ya nane.
Champions League
Kinyang'anyoro cha Champions League kinarejea uwanjani kesho Jumanne na Jumatano. 
Arsenal ya London na Barcelona ni timu mbili ambazo zinawania kupata ushindi wa tatu katika michezo mitatu ya makundi yao.
Viongozi hao wa Premier League Arsenal na Borussia Dortmund makamu bingwa wa Champions League walikabiliana katika msimu wa mwaka 2011-2012 wakati Robin van Persie alipofanikisha ushindi wa Arsenal nyumbani. Mchezo wa pili ulikuwa sare ya bao 1-1 mjini Dortmund.
Schalke 04 pia itakuwa uwanjani kesho Jumanne ikioneshana kazi na Chelsea London . Chelsea inahitaji kwa udi na uvumba ushindi mjini Gelsenkirchen kupata kujiamini zaidi baada ya ushindi wao wa mabao 4-0 dhidi ya Steaua Bucharest katika kundi E. Michezo mingine ni kati ya Steaua Bucharest ikiikaribisha Basel ya Uswisi, Marseille ya Ufaransa inakuwa mwenyeji wa SSC Napoli ya Italia, wakati katika kundi G , Porto ya Ureno imewaalika Zenit St Petersburg ya Urusi. Austria Vienna ina miadi na Atletico Madrid , na Celtic itakuwa kibaruani na Ajax Amsterdam ya Uholanzi katika kundi H, ambapo pia AC Milan inaikaribisha nyumbani Barcelona.
Michezo hiyo inaendelea siku ya Jumatano ambapo mabingwa Bayern Munich inawakaribisha Pilsen ya Denmark na Leverkusen wako nyumbani kuikaribisha Schachtar Donetzk ya Ukraine.

No comments:

Post a Comment