Cristiano Ronaldo ama Zlatan Ibrahimovic mmoja wao atakosa kuonekana
katika fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil kutokana na timu
zao za taifa kupangwa leo kuamua ni timu gani inayostahili kwenda
Brazil. Nafasi nne zimebakia katika bara la Ulaya. Ufaransa imepangwa
kuumana na Ukraine , Ugiriki itakwaana na Romania na Iceland ina kibarua
na Croatia katika michezo ya mtoano kuwania tikiti hizo nne za mwisho
kwa mataifa ya Ulaya. Michezo hiyo itafanyika Novemba 15 na 19.
Watu 16 wanaotokana na ukoo wa waanzilishi wa chama cha kandanda nchini
Uingereza FA, wakitokea kutoka New Zealand na Marekani , watahudhuria
uzinduzi wa sanamu katika uwanja wa Wembley leo kama sehemu ya sherehe
za miaka 150 za chama hicho tangu kuanzishwa.
Chama hicho ambacho ni cha kwanza duniani kuendesha mchezo wa mpira
kiliundwa Oktoba 26, 1863 na chakula cha usiku kitafanyika mjini London
siku ya Jumamosi kuadhimisha tarehe hiyo chama hicho kilipoundwa.
No comments:
Post a Comment