Uamuzi wa Serena Williams kwamba amefadhaishwa na uchezaji wake katika
msimu wa mwaka 2013 unaonesha nia ya mchezaji huyo kutaka kupita kiwango
cha mataji 18 ya Grand Slam ambayo Martina Navratilova na Chris Evert
wamefikia na kuwania kuifikia rekodi ya Steffi Graf wa Ujerumani ya
mataji 22.
Wakati huo huo Rafael Nadal wa Uhispania anashikilia bado nafasi ya
kwanza katika orodha ya wachezaji bora wa tennis kwa wanaume kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na shirikisho la mchezo huo duniani ATP hii leo.
Na kwa taarifa hiyo ndio sina budi kusema tumefikia mwisho wa kuwaletea
habari hizi za michezo jioni ya leo. Jina langu ni Sekione Kitojo , hadi
mara nyingine kwaherini.
No comments:
Post a Comment