Mlinzi wa kati wa Barcelona Carles Puyol amesema yuko tayari kuwakabili Real Madrid katika Clasico ya kwanza ya msimu Jumamosi licha ya kurejea hivi punde kutoka katika maumivu ya mguu ya muda mrefu.
Nahodha huyo wa Barca amerejea baada ya miezi saba ya kuwa kando katika mchezo wa wiki iliyopita dhidi ya Osasuna uliomalizika kwa matokeo ya 0-0.
Na licha ya mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 35 kutokupangwa katika mchezo dhidi ya AC Milan mchezo wa ligi ya mabingwa juzi Jumanne Puyol ana matumaini ya kuwepo fiti katika dimba la Camp Nou huku Gerard Pique akiendelea kusumbuliwa na msuli.

No comments:
Post a Comment