Sir Alex Ferguson akishika nakala ya kitabu cha historia ya maisha yake ya soka huko Tesco Extra kitongoji cha Salford hii leo. |
Mamia ya watu wamekuwa wakikusanyika katika tawi la Tesco lililoko jijini Manchester tangu mapema asubuhi ya leo ili kuweza kupata fursa ya kupata kopi ya kitabu kilichosainiwa na meneja wa zamani wa Manchester United ambacho kinahusu historia ya Sir Alex Ferguson katika soka (autobiography).
Meneja huyo wa zamani wa Manchester United alihudhuria katika tawi moja la duka la vitabu la Tesco
Extra store maeneo ya Salford kuanzia saa tanmo asubuhi kwa lengo la kutia saini vitabu vilivyonunuliwa na wadau kopi ambazo zinaelezea maisha yake kuanzia mwaka 1999 na kuenedelea.
Ferguson mwenye umri wa miaka 71, alijiuzulu mwezi Mei kuiongoza United baada ya miaka 26.
Kupitia kitabu hicho, Ferguson aliikosoa Liverpool na meneja wake wa zamani Rafael Benitez, mchezaji wake wa zamani David Beckham na Roy Keane, na nyota wa sasa Wayne Rooney.
Pia ametanabaisha kuwa mara mbili alipewa ofa ya kuifundisha timu ya taufa ya England.
No comments:
Post a Comment