KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, October 11, 2013

Dereva wa F1 Maria Villota afariki

Dereva mashuhuri mwanamke wa mashindano ya langalanga Formula 1 Maria De Villota amepatikana amefariki ndani ya chumba cha hoteli moja mjini Seville,Hispania.
Msemaji wa polisi alisema.
"Tunachukulia kilikua kifo cha kawaida,lakini hatuwezi kuthibitisha chochote na uchunguzi utafanywa kuhusu kifo chake"
De Villota, aliyekuwa na umri wa miaka 33,alikua dereva wa akiba wa langalanga. Alipofuka jicho lake la kulia katika ajali ya mwezi wa Julai mwaka jana alipokua akifanya mazoezi na timu ya Marussia.
Alipata majeraha mabaya kichwani na usoni baada ya kugongana na lorry katika jimbo la Cambridgeshire, Uingereza lakini aliruhusiwa kuanza tena kuendesha gari.
Iliarifiwa De Villota, binti wa dereva wa zamani wa mashindano ya Formula 1, Emilio De Villota,alikwenda Seville kuzindua kitabu kuhusu maisha yake.
Timu na madereva wa langalanga wameelezea kushtushwa kwao na msiba huo.
Jenson Button wa Uingereza amesema. 
"inasikitisha sana. Msichana huyu amekumbwa na masaibu mengi sana, kupita yale yanayowakumba watu wengi duniani. Ni habari zilizotushtuwa timu nzima na jamii nzima ya mbio za langalanga."
"tulimuona mwaka huu mjini Barcelona.Tukifanya kazi kwa wakfu wa kuwasaidia watoto na alikua wa kwanza kujitolea na kuwashawishi madereva wengi kujiunga nasi.Alikua akichangia mengi kwa jamii ."

No comments:

Post a Comment