KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, October 21, 2013

FAINALI ZA VILABU AFRIKA: AHLY NA PIRATES NA MAZEMBE NA CS SFAXIEN.

Klabu ya soka ya Al-Ahly ya Misri, jana imefanikiwa kutoka kifua mbele katika kutetea ubingwa wao wa ligi ya klabu bingwa Afrika baada ya kuicharaza klabu ya Coton Sport ya Cameroon kwa penalty na kufanikiwa kufika fainali.
Klabu hiyo ya Cairo ilishinda kwa ujumla wa mabao sita saba kwenye mechi iliyochezwa katika eneo la El-Gouna baada ya mechi ukamilia kwa sare ya bao maoja kwa moja.
Matokeo sawa na hayo yalishuhudiwa kwenye mechi ya mkondo wa kwanza, iliyomalizika kwa mabao mawili kwa mawili.
Ahly itakutana na Orlando Pirates wa Afrika Kusini katika fainali itakayokuwa na mikondo miwili mwezi ujao.
Abdullah Al Saied aliingiza bao baada ya dakika tatu ya kuanza kwa mchezo na kuipa Misri mwanzo mzuri wa mechi , na kisha kuingiza bao lengine.
Ahly, ambayo haikushiriki mechi tatu za kimataifa, iliyohusisha mechi ya Misri ambayo ilishindwa vibaya sana na Ghana, ilipata nafasi nzuri za kuendeleza ushindi wao wakati wa kipindi cha kwanza cha mchuano.
Mchezaji Alexis Yougouda alifanikiwa kuingiza bao lake la saba
Wakati wa mchuano huo, Mohamed Aboutrika alikosa bao lake la kwanza lakini wachezaji wenzake walifanikiwa kuingiza mabao baadaye.
Mechi hiyo ilichezwa bila ya mashabiki baada ya kupigwa marufuku kushuhudia mechi za klabu yao, kutokana na ghasia za hivi karibuni.
Kocha wao Mohamed Youssef pia alilazimika kujionea mechi akiwa nje ya uwanja baada ya kuondolewa uwanjani wakati wa mkondo wa kwanza wa mecih hizo mjini Garoua wiki mbili zilizopita.
Ahly wameshinda ubingwa wa ligi hiyo mara saba awali, na kuifanya kuwa klabu yenye kufanikiwa zaidi barani Afrika.

KATIKA KOMBE LA SHISRIKISHO

Kocha wa kikosi cha TP Mazembe ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Patrice Carteron amekipongeza kikosi chake baada ya kufanikiwa kutinga fainali ya kombe la shirikisho baada kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stade Malien ya Mal katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini.

Mazembe ilishinda mchezo huo katika uwanja wa nyumbani uliopigwa Jumamosi baada ya ushindi waq ugenini wa mabao 2-1 na hivyo kutinga hatua hiyo kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1.

 Carteron amekipongeza kikosi chake kwa maneno 
"Michezo hiyo miwili ilikuwa migumu , wachezaji walicheza vizuri lakini kitu muhimu kwangu ilikuwa ni nidhamu waliyoonyesha katika michezo hiyo miwili walicheza kwa moyo.Walikuwa vuzuri sana na najivunia kwa hilo.

"Walijitoa kwa asilimia 100% na walielewa juu ya kufanya kazi na ndio kitu kizuri walichokifanya.
"Haikuwa rahisi kuwashinda Stade Malien. Katika nusu ya pili ya mchezo wa kwanza tulicheza vibaya sana lakini katika mchezo wa pili tulicheza kwa asilimia 100% na tumefuzu kucheza fainali" 
Mazembe iliwakosa wachezaji wake watatu Rainford Kalaba, Stopila Sunzu na Nathan Sinkala.
wachezaji hao walizuiliwa na nchi yao kufuatia kuikimbia mechi dhidi ya Brazil iliyopigwa huko China.

Sasa watakutana dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment