Kifungo cha mjumbe wa zamani wa shirikisho la soka duniani Fifa Amos Adamu cha miaka mitatu sasa kimemalizika.
Mnigeria huyo alihukumiwa kwa kifungo hicho baada ya kudaiwa kudai fedha kwa ajili ya kulipa fadhila ya kupiga kura kwa wenyeji wa kombe la dunia katika fainali za michuano ya 2018 na 2022.
Alionekana pichani akidai dolari za kimarekani $800,000 kabla ya kuondolewa katika zoezi la upigaji kura la mwaka 2010.
Adamu, ambaye kwasasa yuko huru kufanya kazi za mpira wa miguu baada ya adhabu yake kukamilika hapo jana amekaririwa akisema
"Namshukuru mungu adhabu imkwisha . Sina kinyongo na mtu."
“Sasa ni mtu mwingine tena mwerevu kuliko hapo kabla”Amos Adamu
Skendo hiyo ya rushwa na kifungo cha miaka mitatu kwa Adamu ambayo pia iliwakumba wajumbe wengine watano ambao walisimamishwa katika zaozi la upigaji kura ambazo ziliamua Russia
kuwa wenyeji wa fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nao Qatar ikiamualiwa kuandaa fainali za 2022.
No comments:
Post a Comment