KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, October 10, 2013

JORDI ALABA KUIKOSA EL CLASICO

Mlinzi wa kushoto wa BARCELONA Jordi Alaba atakuwa nje  ya uwanja kwa takribani wiki sita kufuatia kurejea katika maumivu ya msuli hizi zikiwa ni taarifa zilizothibitishwa na klabu yake ya Barca.
 
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 24 alikuwa katika hatua ya mwisho mwisho ya kurejea kundini na alikuwepo katika mchezo wa mwezi septemba ambao waliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Sevilla na timu timu ya madaktari ilikuwa imesema zimesalia wiki mbili za kurejea kwake lakini sasa atalazimika kusalia pembeni kwa kipindi hicho.

Sasa anatarajiwa kukosekana katika mchezo wa kwanza wa El Clasico dhidi ya wapinzani wao wakubwa katika soka la Hispania Real Madrid Oktoba 26, pamoja na mchezo dhidi ya AC Milan mchezo wa vilabu bingwa Ulaya.

Taarifa hizi ni pigo kwa kocha Gerardo Martino, ambaye amekuwa na matatizo ya kuwakosa Lionel Messi na Javier Mascherano katika wiki za karibuni.

Barcelona ambayo haijapoteza alama katika Primera Division mpaka sasa wanajipanga na mchezo dhidi ya Osasuna Oktoba 19.

No comments:

Post a Comment