KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, October 28, 2013

LIGI KUU: Azam mbabe dhidi ya Simba uwanja wa taifa.

Katika mfululizo wa michezo ya ligi kuu ya Soka Tanzania bara hii leo Azam FC ya Chamazi imejiweka vizuri katika usukani wa ligi hiyo baada ya kuitandika Simba mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mabao yote mawili yamefungwa na raia wa Ivory Coast Kipre Herman Tchetche na kuipeleka kileleni klabu yake ya Azam kwa kufikisha jumla ya alama 23 na kuwa zaidi ya waliokuwa vinara kwa muda mrefu Simba kwa alama 3 zaidi.
Mpaka kufikia mapumziko timu hizi zilikuwa sare ya bao 1-1 huku Simba ndio waliokuwa wa kwanza kuandika bao la uongozi kupitia kwa Ramadhani Singano baada ya kupata mpira wa pasi ya Zahor Pazi.
Dakikia moja kabla ya mapumziko Kipre Tchetche alisawazisha bao hilo baada ya pasi safi ya mlinzi wa kulia Erasto Nyoni.
Bao na baadaye kufunga bao la pili baada ya kufanya juhudi binafsi za kuwatoka walinzi wa Simba.

Matokeo mengine 

Coast Union 3 vs Mtbwa 0
ruvu 1 vs kagera 1

No comments:

Post a Comment