KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, October 28, 2013

LIGI KUU: JE YANGA ATAZAIDI KUMSHUSHA SIMBA KESHO?

Young Africans kesho watashuka katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kupamabana na maafande wa jeshi la kujenga Taifa Mgambo Shooting kutoka mkoani Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara mzunguko wa 11.
Kikosi cha Young Africans mpaka sasa kimejikusanyia jumla ya pointi 19, kikiwa kimecheza michezo 10, kikishinda michezo 5, sare michezo 4 na kupoteza mchezo mmoja, huku ikiwa ni tofauti ya pointi moja dhidi ya timu tatu zilizopo juu yake Mbeya City, Azam FC na Simba SC zote zina pointi 20.
Kocha mkuu wa Yanga amekua akiendelea kukinoa kikosi chake ambacho kwa sasa kinapigana kuhakikisha kinapata ushindi katika michezo yake yote mitatu iliyobakia na kuweza kuwa juu kileleni kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili.
Yanga kesho itashuka dimbani kusaka pointi tatu muhimu kutoka kwa timu inayoshika mkia Mgambo Shooting na endapo itaibuka na ushindi katika mchezo inaweza moja kwa moja kukwea katika nafasi ya kwanza au ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu kutegemea na matokeo ya michezo ya leo.
Katika mchezo wa kesho wachezaji Nizar Khalfani na David Luhende watakosekana kutokana na kuwa majeruhi, Nizar amechanika nyama za paja (mazoezini) huku Luhende akiendelea na matibabu kufuatia kupata maumivu ya goti katika mchezo dhidi ya Rhino Rangers.
Kiungo Haruna Niyonzima pia ataukosa mchezo huo kutokana na kuomba ruhusa ya siku tatu kwa ajili ya kumaliza matatizo ya kifamilia yanayomkabali, Niyonzima aliondoka jana kuelekea nchin Rwanda na anatarajiwa kurudu siku ya jumatano kuungana na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa siku ya ijumaa dhidi ya JKT Ruvu Stars.
Wapenzi, wanachama na washabiki wa Young Africans mnaombwa kesho kujitokeza kwa wingi katika dimba la Uwanja wa Taifa kuja kuwashangilia vijana watakapokua wanaipeperusha bendera ya jangwani dhidi ya Mgambo katika kusaka pointi tatu muhimu.

No comments:

Post a Comment