Bao la Daniel Sturridge kichwa limeipa Liverpool sare ya na angalau kuponyea chupuchupu kuangushwa na Newcastle uliyomaliza ikiwa na wachezaji 10 uwanjani.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England alitumia vizuri pasi nzuri ya mwisho kutoka kwa Luis Suarez ambaye hakuwa mbinafsi akiwa umbali wa yadi sita na kukiokoa kikosi cha Brendan Rodgers ambao hawakuwa bora hii leo katika dimba la St
James’ Park.
Juhudi za Yohan Cabaye na kufanikiwa kuupeleka chini mpira uliozaa goli na kumpita mlinda mlango wa Simon Mignolet ziliwapa Newcastle bao la uongozi dakika ya 23 kipindi cha kwanza.
Moussa Sissoko alikaribia kuwaandikia wenyeji bao la pili lakini mpira wake uliokolewa na Mignolet, huku Suarez akikaribia kusawazisha kwa kichwa kabla mpira huo kuokolewa katika mstari wa goli na Davide Santon.
Liverpool ilishindwa kupata bao la mkwaju wa penati kupitia kwa Steven Gerrard dakika tano kabla ya mapumziko baada ya Mapou Yanga-Mbiwa kumfanyia madhambi Suarez, ambaye huenda angekuwa ameotea wakati wa kutengeneza mashambulizi.
Paul Dummett aliendelea kuwapa uongozi Magpies dakika 10 baada ya mapumziko lakini Sturridge akasawazisha zikiwa zimesalia dakika 20 mchezo huo kumalizika.
Matokeo mengine
Newcastle United
| - |
Liverpool
| (1-1) | |||||||
Swansea
| - |
Sunderland
| (0-0) | |||||||
Stoke
| - |
West Bromwich Albion
| (0-0) | |||||||
Manchester United
| - |
Southampton
| (1-0) | |||||||
Everton
| - |
Hull
| (1-1) | |||||||
Chelsea
| - |
Cardiff
| (1-1) | |||||||
Arsenal
| - |
Norwich
| (1-0) | |||||||
No comments:
Post a Comment