Uchaguzi
wa Bodi ya Ligi Tanzania (Tanzania Professional League- TPL Board)
unafanyika kesho kwenye ukumbi wa mikutano uliopo
Golden Jubilee Tower kuanzia saa 3 asubuhi.
Mgeni
rasmi katika mkutano huo wa Bodi ya TPL ambao unafanyika kwa mara ya
kwanza atakuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Leodegar Tenga.
Kwa
mujibu wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, wajumbe wanaounda Mkutano wa
Uchaguzi ni wenyeviti kutoka klabu 24 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL), na
14 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Viongozi
wa klabu za FDL wamefikia hoteli ya Royal Valentino iliyoko Barabara ya
Uhuru wakati wale wa VPL ambao pia watashiriki Mkutano Mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wamefikia hoteli ya Landmark
iliyopo Ubungo.
Wagombea
kwenye uchaguzi huo ni Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti), Said Muhammad
Said Abeid (Makamu Mwenyekiti) wakati wanaoumba ujumbe wa Kamati ya
Uendeshaji ni Khatib Omari Mwindadi na Kazimoto Muzo
No comments:
Post a Comment