Serikali
ya Kenya imesema haina fedha kwaajili ya kuandaa Michuano ya Chalenji
ya mwaka huu ambayo imepangwa kupigwa Novemba 27 hadi Desemba 12
Nairobi,Kenya.
Tamko hilo ni pigo zito
waandaaaji wa michuano hiyo ambao ni Baraza la Vyama vya Soka la Nchi za
Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) lililo chini ya Rais Leodegar Tenga
na Katibu Mkuu wake Nicholas Musonye.
Awali, Mwenyekiti wa
Shirikisho la Soka Kenya(FKF), Sam Nyamweya alitangaza kuwa,michuano
hiyo itaandaliwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya shirikisho lake na
Serikali ya nchi hiyo.
Katibu wa Baraza la
Michezo la Kenya,Hassani Wario alisema, Serikali yake haitashiriki
katika kuandaa michuano hiyo kutokana na ufinyu wa bajeti yake kwa
sasa.
“Kuandaa tukio kama hili kunahitaji fedha nyingi ambazo Serikali haina kwa wakati huu.
“Ni lazima tuwe wa
kweli, hatuwezi kuungana na FKF na kudhamini mashindano hayo kwasababu
hatuna bajeti kwaajili hiyo,”alisema Waria na kuongeza:
“Kuna vyama vingine ambavyo vinahitahi fedha kama ilivyo soka, kuogelea, wavu na hata Hockey, ni vigumu kujikita katika soka tu.
Hata hivyo, Musonye akizungumza na Mwananchi alisema:
“Tumeamua na ni lazima michuano hii ifanyike Kenya.
“Tunatafuta wadhamini
wengine, lakini ninachoweza kukuhakikishia ni kwamba mashindano
yatafanyika hapa na hayawezi kuhamishiwa sehemu nyingine.
Mara ya mwisho Kenya iliandaa michuano ya Chalenji mwaka 2009 ambapo Uganda ilifanikiwa kutwaa ubingwa.
SOURCE: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment