Hamad
Yahya Juma wa Mtibwa Sugar ndiye Mwenyekiti wa kwanza wa Bodi ya Ligi
Tanzania (Tanzania Professional League- TPL Board) baada ya kushinda
katika uchaguzi uliofanyika leo mchana (Oktoba 25 mwaka huu) kwenye
ukumbi wa mikutano uliopo Golden Jubilee Tower, Dar es Salaam.
Juma
ambaye hakuwa na mpinzani alipata kura zote kumi za ndiyo zilizopigwa
na klabu za Ligi Kuu zilizohudhuria mkutano huo. Klabu ambazo
hazikuhudhuria uchaguzi huo ni JKT Ruvu, Mgambo Shooting, Coastal Union
na Rhino Rangers.
Naye Said Muhammad Said Abeid ambaye pia hakuwa na mpinzani amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kupata kura zote za ndiyo.
Kwa
upande wa wajumbe wawili wa Kamati ya Uendeshaji, wote Kazimoto Miraji
Muzo wa Pamba na Khatib Omari Mwindadi wa Mwadui wameshinda kwa kura
zilizopigwa na klabu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Muzo
alipata kura 15 za ndiyo wakati mbili zikimkataa, huku Mwindadi akipata
kura 16 na moja ilimkataa. Klabu za FDL ambazo hazikuhudhuria uchaguzi
huo ni Transit Camp, Burkina Faso, Polisi Mara, Stand United, Toto
Africans, Polisi Tabora na Kanembwa JKT.
No comments:
Post a Comment