TUNAFURAHI KUSIKIA AJENDA- TENGA
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) anayemaliza muda wake,
Leodegar Tenga amesema amefurahishwa na jinsi kampeni za uchaguzi
zinazokwenda kutoka na ukweli kuwa wagombea wamekuwa wakielezea kile
wanachotaka kuufanyia mpira wa miguu.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye ofisi za TFF leo mchana, Rais Tenga
ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF) amesema Watanzania wanataka kusikia ajenda za
wagombea.
“Ombi
langu ni kwamba kampeni zimeanza vizuri, watu wanazungumza hoja zaidi.
Ni jukumu la wajumbe kupima na kufanya uamuzi. Kwangu mimi
nimejitayarisha kumkabidhi Katiba, Rais mpya wa TFF,” amesema.
Tenga
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika
Mashariki na Kati (CECAFA) amesema kazi kubwa iliyofanywa na uongozi
wake ni kujenga taasisi (TFF) pamoja na kuweka mifumo (structure)
inayoainisha majukumu ya kila mmoja.
“Ajenda
yetu wakati tunaingia madarakani mwaka 2005 ilikuwa ni kujenga taasisi.
Tayari taasisi ipo, sasa mtazamo uwe kuushughulia mpira wa miguu
wenyewe,” amesema.
Mkutano
Mkuu wa TFF unafanyika kesho kwenye ukumbi wa mikutano wa NSSF
Waterfront, na tayari wajumbe wa mkutano huo ambao pia utakuwa na ajenda
ya uchaguzi siku inayofuata wameshawasili jijini Dar es Salaam.
Wawakilishi
kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ashford
Mamelodi ambaye ni Ofisa Maendeleo wa kanda hii, Magdi Shams El Din
ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF na Rais wa Chama cha Mpira
wa Miguu Zanzibar (ZFA) ni miongoni mwa wageni watakaohudhuria mkutano
huo.
No comments:
Post a Comment