Kiungo wa Bayern Munich Thiago Alcantara amerejea katika mazoezi mepesi baada ya kusumbuliwa na kifundo.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 22 alipatwa na maumivu katika mchezo wake wa pili wa mabingwa Ulaya baada ya kuhamia katika klabu hiyo akitokea Barcelona kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 21.6.
Manchester United ilikuwa ikihusishwa na kumtaka Thiago lakini aliamua kujiunga na bosi wake wa zamani wa Barca Pep Guardiola.
Bado haijafahamika ni lini atarejea uwanjani.
No comments:
Post a Comment