KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, November 9, 2013

Ahly na Pirates nani kubwa klabu bingwa Afrika kesho?

Bingwa mtetezi wa vilabu bingwa Afrika Al Ahly wanatarajiwa kuitumia faida ndogo ya goli la ugenini hapo kesho kufuatia kumaliza mchezo kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 wiki iliyopita iliyopita dhidi ya Pirates ya huko.
Pia watakuwa na faraja kubwa baada ya kuruhusiwa kucheza mchezo huo katika jiji kubwa la nchi ya Cairo, ndani ya uwanja wenye uwezo wa kukusanya watazamaji 30,000 wa Arab Contractors.
Itakumbukwa kuwa Ahly walikuwa nje ya jiji la Cairo tangu mwezi April kufuatia sababu ndogo za hofu ya kiusalama ndani ya jiji hilo.
Hata hivyo bingwa huyo mara saba wa vilabu Afrika walivunjika moyo na bao la kusawazisha la wenyeji wao katika mchezo wa kwanza katika dakika za majeruhi mjini Soweto na huku Pirates wakielekea Cairo hiyo kesho wakiwa na ahadi ya kupigana kufa kupona ili kuibika na ushindi na hatimate kutwaa taji ndani ya ardhi ya Misri.
Orlando Pirates kutoka Afrika kusini walifanikiwa kutinga fainali baada ya kupata faida ya bao la ugenini dhidi ya Esperance ya Tunisia baada ya timu zote kumaliza mchezo kwa suluhu 0-0 katika mchezo wa kwanza wakiwa nyumbani Soweto.

Mshambuliaji wa Pirates Lennox Bacela amenukuliwa akisema
Timu zote zina dakika 90 za kuamua, tutaona nani zaidi baada ya mchezo
Kauli ya Lennox Bacela inaungwa mkono na nyota wa Ahly Wael Gomaa ambaye ameonya kuwa Pirates wanacheza vizuri na hivyo hawapaswi kuwakuchukulia kwa urahisi.
"Pirates wanacheza vizuri wanapokuwa ugenini, na goli lao la dakika ya mwisho litatupa wakati mgumu katika mchezo wa pili"


Ahly walionyesha uzoefu wao katika mchezo wa kwanza na walipata bao lao la uongozi kupitia kwa Mohamed Aboutrika dakika ya 14
Pirates watakumbwa na pigo kubwa kesho kwa kuwakosa nyota 'skipper' Happy Jele na Andile Jali ambao wana adhabu ya kusimama mchezo mmoja baada ya kuonyeshwa kadi za manjano katikia mchezo wa kwanza.
Kukosekana kwa Jele sasa kunafungua mlango kwa 'skipper' mwingine Lekgwathi kuingizwa katika kikosi cha kwanza, naye kiungo Lehlohonolo Masalesa akitarajiwa kuziba pengo la kiungo nyota Jali.
Bingwa wa vilabu bingwa Afrika atapokea zawadi ya dolari za kimarekani $1.5 na atakuwa na tikiti ya kucheza michuano ya vilabu bingwa dunia ambazo fainali zake zitapigwa nchini Morocco mwezi Desemba.

No comments:

Post a Comment