KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, November 23, 2013

HAMISI 'DIEGO' KIIZA AONGEZWA NA KOCHA MICHO NDANI YA KIKOSI CHA UGANDA CRANES.

Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Uganda (Uganda Cranes) Mulitin ‘Micho’ Sredojevic ametangaza kuwaongeza wachezaji watatu wanaocheza soka nje ya nchi ya Uganda katika kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 20 kuelekea katika michuano ijayo ya GOtv Cecafa Challenge Cup ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Novemba 27.
Miongoni mwa wachaji hao watatu walioitwa ni pamoja na  wachezaji wawili wanaochezea soka nchini Kenya Aucho Khalid na mshambuliaji Daniel Sserunkuma kutoka katika vilabu vya Tusker FC na Gor Mahia FC pamoja na mshambuliaji wa Young Africans SC ya Tanzania Hamis ‘Diego’ Kiiza.
Licha ya hapo kabla kuweka mpango wa kutaka kuwatumia wachezaji wanaocheza soka nchini Uganda pekee ili kujiandaa vema na michuano ya wachezaji wa ndani barani Afrika CHAN nchini Afrika kusini mwezi Januari, Micho amesema wachezaji wachache wanaocheza soka nje ya nchi wataweza kukiweka kikosi chake vizuri zaidi na kuongeza motisha kwa wale wanaocheza soka nchini Uganda.
Kikosi hicho kimemjumuisha Geoffrey ‘Baba’ Kizito ambaye alikuwemo kikosini mwezi Septemba katika mchezo dhidi ya Senega.Kwasasa Baba Kizito ni mchezaji huru baada ya utumishi wake katika klabu moja huko Vietnam kufikia tamati.
Winga mkongwe Vincent Kayizzi amerejeshwa kikosini licha ya kiwango kibovu alichoonyesha katika mchezo wa hivi karibuni dhidi ya Rwanda'Amavubi' mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliiopigwa mwishoni mwa juma uwanja wa Namboole.
Mlinda mlango wa SC Victoria University Benjamin Ochan amepata nafasi kikosini kama ilivyo kwa Julius Ntambi (Kiira Young) na Franco Oringa (Bidco FC).
Kikosi hicho kina walinda mlango watatu, walinzi nane, viungo sita, na washambuliaji watatu ambao wanatarajiwa kuondoka nchini humo Jumatatu wakiwa na viongozi watano.

Kocha Mulitin 'Micho' Sredojevic (Head Coach), Kefa Kisala (Assistant Coach), Fred Kajoba (Goal keeping Coach), Crispus Muyinda (Manager) and Dr. Ronald Kisolo plus Media officer Kenneth Muwanga.

Uganda Cranes wako kundo moja la C na Rwanda, Sudan na Eritrea na wataanza kampeni ya kutetea taji Ijumaa ya tarehe 29 dhidi ya Rwanda.

Full squad: 
Goalkeepers: Ochan Benjamin (SCVU), Ismail Watenga (Viper SC) and Franco Oringa (Bidco FC)
Defenders: Julius Ntambi (Kiira), Nicholas Wadada (Vipers SC), Isaac Muleme (SCVU), Godfrey Walusimbi (SC Villa), Richard Kasagga (Kiira),  Savio Kabugo (SCVU),  Ibrahim Kizza (KCC FC), Martin Mpuga (SCVU)
Midfielders: Khalid Aucho (Tusker FC), Geoffrey ‘Baba’ Kizito (unattached), Said Kyeyune (URA FC), Joseph Mpande (Vipers SC), Brian Majwega (KCC FC) and Vincent Kayizzi (Vipers SC)
Strikers: Hamis ‘Diego’ Kiiza (Yanga), Emmanuel Okwi (SC Villa) and Dan Sserunkuma (Gor Mahia FC)

No comments:

Post a Comment