Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amesema kuwa mara kadhaa amekuwa akitakiwa na vilabu mbalimbali ambavyo vimekuwa vikitaka huduma yake.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina amekuwa akiitumikia Camp Nou tangu akiwa mtoto kwasasa yuko ndani ya mkataba ambao utamuweka hapo mpaka Juni 2018, lakini hiyo haikatishi tamaa vilabu vingine kumtaka.
Pia mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amekuwa akisisitiza kuwa yeye ni mwenye furaha katika klabu yake ya Catalunya na anajiandaa kusaka majibu ya kwanini angependelea kumalizia kazi yake ya uchezaji soka ndani ya Barcelona.
"Nijiona ni mwenye heshima kila mara jina langu likitajwa na vilabu vingine vikubwa. Ni kweli kwamba wengi wanaonyesha nia kwangu" the talismanic No.10 alikuwa akiongea na De Telegraaf.
"Lakini maoni yangu hayajabadilika. Aina ya uchezaji wa Barcelona inanifaa na ni ndoto yangu kusalia Barcelona 'for the rest of my life. "
Messi kwasasa yuko katikati ya kipindi cha miezi miwili ya kusalia benchi akiuguza jeraha na anaamini timu yake inaweza kufanya vema bila ya uwepo wake.
No comments:
Post a Comment