Mabingwa watetezi Bayern Munich na mabingwa mara tisa Real Madrid ni
miongoni mwa timu nne zinazolenga kupata ushindi wa nne mfululizo wa
Champions League wiki hii ili kujikatia tikiti ya kucheza awamu ya
mchujo.
Paris St Germain na Atletico Madrid pia zimeshinda mechi zote tatu, huku
Manchester City, ambao wameshinda mbili na kushindwa moja, wanaweza pia
kujikatia nafasi ya hatua ya mchujo kama wataiwashinda CSKA Moscow
katika kundi D.
Barcelona, ambao wameangusha pointi mbili, watafuzu kama watashinda
nyumbani dhidi ya AC Milan katika kundi H nao Manchester United watapiga
hatua kubwa ya kufikia awamu hiyo kama watawapiku Real Sociedad.
Bayern watakuwa ugenini dhidi ya Viktoria Plzen, wakati nao Paris St
Germain wakicheza nyumbani na Anderlecht.
Real Madrid wanaelekea kwa
watani wao wa jadi Juventus huku nao Atletico Madrid wakiwakaribisha
Austria Vienna. Shakhtar Donetsk watakuwa na kibarua dhidi ya Bayer
Leverkusen, wakati nao FC Copenhagen wakiangushana na Galatasaray.
Olympiakos watafunga kazi na Benfica.
Katika mechi nyingine za Jumatano Basel watapambana na Steaua Bucharest,
Chelsea wawakaribishe Schalke 04, wakati nao Borussia Dortmund wakiwa
wenyeji wa Arsenal. Napoli watakuwa wenyeji wa Olympique Marseille.
Zenit St Petersburg watapimana nguvu na Porto nao Ajax Amsterdam wacheze
na Celtic.
No comments:
Post a Comment