Tottenham Hotspur wanasisitiza kuwa golikipa wao anaweza cheza licha
ya kugongwa kichwa ugenini Everton kufuatia shutuma kali kwa kukosa
kumwondoa uwanjani kwenye sare yao tasa Jumapili.
Spurs walikashifiwa na mkuu wa matibabu katika shirikisho la kandanda
duniani, Fifa na wakereketo wa ustawi wa wachezaji kwa kukubali Lloris
kubakia mchezoni licha ya mtikiso kichwani baada ya kugongana na
mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku.
Lakini Spurs katika taarifa walioitoa Jumatatu walisema, “Klabu
kinadhibitisha kwamba Lloris alipigwa picha ya kichwa (CT Scan) na
akapewa idhibati na alisafiri kurudi London (Jumapili) usiku.
“Golikipa huyo wa Ufaransa alijeruhiwa kichwani baada ya kugongana
na akapewa idhini ya kuendelea na mchezo baada ya kuchunguzwa na
watabibu wa klabu.”
Mkuu wa matibabu Tottenham, Wayne Diesel, aliongeza, “Baada ya
uchunguzi unaofaa kutekelezwa, tuliridhika kuwa alistahili kuendelea
kucheza.”
Mapema Profesa, Jiri Dvorak, ambaye ni mkuu wa matibabu Fifa,
aliambia chombo cha habaro, Press Association, kuwa, “Mchezaji huyo
alifaa kupumzishwa. Ikiwa mchezaji mwingine mhusika (Lukaku) alhitaji
barafu kwa goti lake, inamaanisha kwamba pigo hilo lilikuwa kubwa.”
“Ni dhahiri asilimia 99 kwamba kupoteza fahamu katika tukio kama hilo kunasababisha mtikiso.”
No comments:
Post a Comment