KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, November 13, 2013

Michael Carrick nje wiki sita.

Kiungo wa Manchester United na England Michael Carrick atakosekana kwa wiki kufuatia kupata maumivu ya msuli maarufu kama Achilles tendon.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 ambaye alicheza dakika zote za mchezo wa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Arsenal Jumapili iliyopita tayari ameshaondolewa katika kikosi cha England kinachojipanga kwa mchezo dhidi ya Ujerumani na Chile.
Wiki hizo sita zitamuweka Carrick nje mpaka baada ya Christmas, na atakosa michezo sita ya ligi ya England.
Carrick hakuwepo katika mchezo wa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fulham Novemba 2 kutokana na matatizo hayo.
Ukiacha mchezo huo mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham na West Ham hajakosa michezo wowote wa mabingwa hao watetezi wa taji la ligi mpaka kufikia sasa.
Carrick atakosa mchezo dhidi ya Spurs Desemba mosi na ataendelea kuwa nje wakati United watakapo kuwa wakiwafuata West Ham Desemba 21.
United pia watakuwa na michezo dhidi ya Cardiff, Everton, Newcastle na Aston Villa kuelekea wiki sita zijazo pamoja na michezo muhimu miwili ya klabu bingwa Ulaya hatua ya makundi pamoja na mchezo wa robo fainali ya Capital One dhidi ya Stoke.
Nyota wa kimataifa wa Belgium Marouane Fellaini, aliyejiunga na klabu hiyo akitokea Everton kwa thamani ya pauni milioni £27.5 mwezi September, pia atakuwa akifikiriwa kuwemo kikosini.

No comments:

Post a Comment