KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, November 13, 2013

MSAIDIZI WA MOURINHO APEWA MIKOBA YA KUINOA MIDDLESBROUGH

Middlesbrough imemtaja meneja msaidizi wa zamani wa Real Madrid Aitor Karanka kama mkuu mpya wa benchi la ufundi kwa mkataba ambao utamalizika 2016.
Karanka mwenye umri wa miaka 40, aliwahi kufanya kazi chini ya Jose Mourinho kwa miaka mitatu ndani ya viunga vya Bernabeu, lakini hajawa bado na uzoefu wa kama meneja.
Mlinzi huyo wa zamani wa Real na Hispania aliondoka kwa mabingwa hao mata tisa wa Ulaya wakati Carlo Ancelotti alipochukua urithi wa kuiongoza timu hiyo kutoka kwa  Mourinho kama maneja wakati wa kiangazi.

Karanka ni nani?

Middlesbrough manager Aitor Karanka (left) working as assistant to Real Madrid manager Jose Mourinho
  • Alizaliwa Vitoria, nchini Hispania mwaka 1973
  • Akiwa kama mlinzi alifanikiwa kuichezea Hispania mchezo mmoja na kabla ya hapo alikuwa akiichezea Athletic Bilbao na Real Madrid akichezea pia Colorado Rapids
  • Amekuwa msaidizi wa Jose Mourinho viungani Bernabeu kuanzia 2010 mpaka 2013
Anakuwa bosi wa kwanza wa Middlesbrough kutoka nje ya England. 
Amenukuliwa akisema
"Hii ni siku muhimu kwangu ninafuraha kujiungta na klabu ambayo yenye kila kitu na mashabiki"
"Ni muda wangu na najua niko tayari. Nimefanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu na Jose na alikuwa akisaidia kila siku na nimejifunza sana.
"Nimezungumza naye na amenitaka nije hapa ana niamini sana katika hili."
Meneja wa zamani wa klabu hiyo Tony Mowbray aliiacha klabu hiyo kutoka pande za Riverside mwezi uliopita na tangu wakati huo msaidizi wake Mark Venus amekuwa akifanya kazi hiyo kwa muda.
Kwasasa Middlesbrough wako katika nafasi ya 16 katika msimamo wa ligi ndogo ya pili kwa ukubwa nchini England ya Championship.
Itakumbukwa miaka saba iliyopita Middlesbrough ilifikia fainali ya Uefa Cup kabla ya kupoteza kwa Sevilla mchezo uliokuwa wa mwisho wa Steve McClaren kabla ya kupindukia katika umeneja.
.

No comments:

Post a Comment