KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, November 7, 2013

STEPHEN GERARD ANA WASIWASI NA LUIS SUAREZ.

 Steven Gerrard anasema Luis Suarez huenda akaondoka Liverpool majira ya kiangazi endapo Liverpool itashindwa kufuzu kucheza Ligi ya mabingwa Ulaya.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay ambaye amefunga jumla ya mabao ndani ya ligi kuu baada ya kushuka dimbani katika michezo mitano anaonekana kuwa mwenye mashaka makubwa ya kuondoka Anfield mwishoni mwa msimu.
Itakumbukwa Suarez alishawishiwa kusalia ndani ya klabu hiyo na bosi wa Liverpool Brendan Rodgers baada ya mpango wa pauni £40 kushindwa kufikiwa na vilabu mojawapo ikiwa ni  Arsenal, ambapo sasa amerejea katika kiwango chake ndani ya msimu huu.

Pia Gerrard amekaririwa akisema
'Luis yuko katika kiwango kizuri. Timu inacheza vizuri, haitakuwa tatizo mwezi Januari.
'Kiangazi ijayo, nadhani itategemea na Liverpool itafanya nini na nini kinaendelea katika mawazo ya Luis.
'Magoli yake na kiwango chake itakuwa ndio ufunguo wa kama tutamaliza katika moja ya nafasi za juu nne.' 
Wakati hayo yakiwa hivyo, Suarez anatarajiwa kuwepo katika mchezo wa Liverpool dhidi ya Fulham Jumamosi baada ya kufikia muafaka na chama cha soka cha Uruguay (UFA). 
Uruguay watakabiliana na Jordan katika mchezo wa mkondo wa kwanza ukiwa ni mchezo wa mtoano wa nyumbani na ugenini (play-off) mchezo ambao utapigwa Mshariki ya kati Jumatano na kwa mujibu wa sheria za shirikisho la soka duniani FIFA ni kwamba Suarez alipaswa kutolewa na klabu yake kwa majukumu ya kimataifa siku tano kabla ya mchezo.
Lakini wakati hayo yakiwa hivyo ni kwamba mwenyewe Suarez alipoulizwa juu ya kufanya majukumu yote mawili kwa pamoja yaania aanze kuichezea Liverpool Jumamosi dhidi ya Fulham na baadaye kuelekea mshariki ya kati amekubali kufanya hivyo. Liverpool italazimika kumpatia mchezaji huyo ndege binafsi mpaka Istanbul kufuatia mchezo huo wa Jumatano.
Mchezo wa pili wa "play-off" utafanyika Montevideo Jumatano ya Novemba 20 ikiwa ni siku tatu kabla ya Merseyside derby dhidi ya Everton mchezo ambao utapigwa Goodison Park, ambapo Suarez atalazimika kusafiri mile 7,000.

No comments:

Post a Comment